• HABARI MPYA

  Saturday, April 14, 2018

  SAMATTA APIGA KAZI YA MAANA, GENK YALAZIMISHA SARE 2-2 UGENINI UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, CHARLEROI
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza kwa dakika 75, klabu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 2-2 na wenyeji, Sporting Charleroi katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa du Pays de Charleroi mjini Charleroi.
  Wenyeji walitangulia kwa mabao mawili ndani ya nusu saa ya kwanza, Kaveh Rezaei akifunga la kwanza kwa penalty dakika ya 11 na Mfaransa Marco Ilaimaharitra akifunga la pili dakika ya 22. 
  Genk wakazinduka na kupata bao la kwanza kabla ya mapumziko mfungaji kiungo Msenegali, Ibrahima Seck dakika ya 36 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake, Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero.
  Mbwana Samatta akimiliki mpira mbele ya beki wa Sporting Charleroi jana Uwanja wa du Pays de Charleroi 

  Na baada ya kuanza kipindi cha pili, Genk wakiongozwa vizuri na Samatta katika eneo la ushambuliaji, walifanikiwa kuoata bao la kusawazisha ndani ya dakika 14, lililofungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Dieumerci N'Dongala kwa pasi ya Pozuelo tena.
  Hiyo inakuwa mechi ya 82 kwa Nahodha huyo wa Taifa Stars, Samatta tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
  Kikosi xha Charlerloi kilikuwa; Mandanda, Martos, Rezaei/Bedia dk90, Diandy, Benavente/Semedo dk82, Marinos, Baby, Dessoleil, Nurio, Ilaimaharitra na Fall/Pollet dk71.
  KRC Genk; Vukovic, Uronen/Maehle dk71, Colley, Aidoo, Mata, Malinovskyi, Seck, Pozuelo, Trossard, Ndongala/Buffalo dk87 na Samatta/Karelis dk75.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA APIGA KAZI YA MAANA, GENK YALAZIMISHA SARE 2-2 UGENINI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top