• HABARI MPYA

  Wednesday, April 18, 2018

  SAMATTA ABADILISHWA BAADA YA SAA MOJA GENK IKITOA SARE YA 0-0 UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, CHARLEROI
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumanne amecheza kwa dakika ya 65, klabu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, AA Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Ghelamco-Arena mjini Gent.
  Samatta alipambana kwa dakika zote 65 kabla ya kubadilishwa, nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis ambaye naye hakuweza kwenda kubadili matokeo.
  Hiyo inakuwa mechi ya 83 kwa Nahodha huyo wa Taifa Stars, Samatta tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Mbwana Samatta (kushoto) akimiliki mpira mbele ya beki wa AA Gent Uwanja wa Ghelamco-Arena mjini Gent 

  Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
  Kikosi cha AA Gent kilikuwa; Kalinic, Gigot, Verstraete, Christiansen/Chakvetadze dk79, Janga/Kalu dk45, Yaremchuk, Dejaegere/Andrijasevic dk45, Asare, Bronn, Simon na Foket.
  KRC Genk; Vukovic, Uronen/Nastic dk43, Colley, Aidoo, Maehle, Seck, Malinovskyi, Pozuelo, Trossard, Samatta/Karelis dk65 na Ndongala/Buffel dk84.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ABADILISHWA BAADA YA SAA MOJA GENK IKITOA SARE YA 0-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top