• HABARI MPYA

    Saturday, April 14, 2018

    SALAH AKABANA NA DE BRUYNE TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA PFA

    WASHAMBULIAJI Kevin De Bruyne na Mohamed Salah wanachuana vikali kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA).
    Nyota hao wa Manchester City na Liverpool wamo kwenye orodha moja na wachezaji wengine, Harry Kane, Leroy Sane, David De Gea na David Silva kuwania tuzo hiyo.
    Eden Hazard, Roberto Firmino na Raheem Sterling ni miongoni mwa majina makubwa yaliyokosekana kwenye orodha ya wawania tuzo hiyo.
    Zoezi hili huhusisha klabu 92 za Ligi mbalimbali England na wachezaji wote wanapiga kura kwa sharti tu la kutomchagua mchezaji anayecheza naye timu moja kwa sasa na kuzikusanya kwa mwakilishi wa PFA kwenye viwanja vyao vya mazoezi.
    De Bruyne na Salah wanapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo kufuata nyayo za mshindi wa 2016-2017, N'Golo Kante.
    Mbelgiji De Bruyne amekuwa mchezaji nyota kwenye kikosi cha Manchester City msimu huu, akifunga mabao saba na kuseti 15 kwenye mechi 32 za Ligi Kuu ya England alizocheza msimu huu.
    Mpinzani wake mkuu katika tuzo hiyo, Salah kwa sasa anaongoza kwa mabao yake 29 alyofunga Liverpool baada ya kuwasili akitokea Roma.
    Mtajwa mwingine kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo, Harry Kane anazidiwa mabao manne tu na Mmisiri huyo kwenye chati ya ufungaji ambaye pia kwa sasa amekata rufaa kuomba apewe bao la pili la Spurs dhidi ya Stoke City Jumamosi iliyopita.
    Orodha ya mwisho inamaanisha kwamba Kane na Salah wapo kwenye nafasi ya kushinda Kiatu cha Dhahabu na Ucheza Bora wa Mwaka wa PFA. 

    Mohamed Salah anachuana na Kevin De Bruyne kuwania tuzo ya PFA PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA PFA 

    Kevin De Bruyne (Manchester City)
    Mabao: 7
    Pasi: 15 
    Mohamed Salah (Liverpool)
    Mabao: 29
    Pasi: 9 
    Leroy Sane (Manchester City)
    Mabao: 9
    Pasi: 12
    Harry Kane (Tottenham)
    Mabao: 25
    Pasi: 2 
    David Silva (Manchester City):
    Mabao: 8
    Pasi: 11
    David De Gea (Manchester United)
    Mechi: 32
    Mabao aliyofungwa: 25

    WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI WA MWAKA WA PFA 

    Leroy Sane (Manchester City)
    Mabao: 9
    Pasi: 12
    Raheem Sterling (Manchester City)
    Mabao: 16
    Pasi: 8  
    Harry Kane (Tottenham)
    Mabao: 25
    Pasi: 2 
    Ederson (Manchester City)
    Mechi: 32
    Mabao aliyofungwa:  24
    Marcus Rashford (Manchester United)
    Mabao: 6
    Pasi 5
    Ryan Sessegnon (Fulham)
    Mabao: 14
    Pasi:  6

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH AKABANA NA DE BRUYNE TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA PFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top