• HABARI MPYA

    Friday, April 13, 2018

    SALAH ABEBA TUZO YA MCHEZAJI KWA REKODI ENGLAND

    WASHINDI WALIOTANGULI  

    August - Sadio Mane
    September - Harry Kane
    October - Leroy Sane
    November - Mohamed Salah
    December - Harry Kane
    January - Sergio Aguero
    February - Mohamed Salah
    March - Mohamed Salah
    MSHAMBULIAJI Mohamed Salah ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England kwa mwezi Machi baada ya kuendelea kufanya kazi nzuri Liverpool.
    Hii inakuwa nara ya tatu kwa msimu huu pekee nyota huyo wa Misri huyo kutwaa tuzo hiyo, baada ya kuchukua pia miezi ya Novemba mwaka jana na Februari, mwaka huu.
    Tangu amerejea England msimu huu akijiounga na kikosi cha Jurgen Klopp cha Liverpool, mchezajhi huyo mwenye umri wa miaka 25 anaonekana mchezaji tofauti kabisa na yule aliyekuwa Chelsea ya hapa pia, kati ya mwaka 2013 na 2015
    Salah pia amevunja rekodi ya Didier Drogba ya mchezaji kutoka Afrika kufunga mabao mengi kwa msimu baada ya kufunga bao la ushindi dakika za lala salaam, Uwanja wa  Selhurst Park dhidi Crystal Palace.
    Naye kocha wa Burnley, Sean Dyche ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Machi, wakati Jamie Vardy wa Leicester City ameshinda tuzo ya Bao Bora la Mwezi Machi.
    Dyche ameiwezesha Burnley kushinda mechi zake zote za mwezi akianza na Everton, West Ham na West Brom, wakati Jamie Vardy ametwaa tuzo hiyo baada ya vao lake zuri alilofunga dhidi ya West Bromkwch Albion kwenye ushindj wa 4-1 Machi 10.

    Mohamed Salah ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England
     PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH ABEBA TUZO YA MCHEZAJI KWA REKODI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top