• HABARI MPYA

  Friday, April 13, 2018

  RUVU SHOOTING YAIADHIBU AZAM FC, YAICHAPA 2-0 MABATINI…’MIKONO 100 AGEUKA SHATI’

  Na Mwandishi Wetu, MLANDIZI
  MABAO ya Khamis Mcha ‘Vialli’ na Fully Zulu Maganga yameipa Ruvu Shooting ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Mcha alianza kuiadhibu timu yake ya zamani kwa bao la mpira wa adhabu kipindi cha kwanza, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Mgambo JKT ya Tanga, Maganga kufunga la pili kipindi cha pili.
  Kipa Mghana wa Azam FC, Razack Abalora aliye katika msimu wake wa kwanza Chamazi tangu awasili kutoka kwao, leo alifungwa kwa urahisi Uwanja wa Mabatini mabao yote mawili dakika ya 29 na 80.
  Matokeo hayo yanaiongezea Ruvu Shooting pointi tatu na kufikisha 29 baada ya kucheza mechi 24 na kupanda hadi nafasi ya nane, kutoka ya 10.
  Azam FC inayobaki na pointi zake 45 baada ya kucheza mechi 24 pia, inaendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 47 za mechi 22 na vinara Simba SC, wenye pointi 55 za mechi 23. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAIADHIBU AZAM FC, YAICHAPA 2-0 MABATINI…’MIKONO 100 AGEUKA SHATI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top