• HABARI MPYA

    Friday, April 13, 2018

    NIKO KOVAC NDIYE KOCHA MPYA BAYERN MUNICH

    KLABU ya Bayern Munich imemthibitisha mchezaji wake wa zamani, Niko Kovac atakuwa kocha wa timu hiyo ya Allianz Arena kuanzia Julai 1.
    Mabingwa hao wa Bundesliga wamekuwa wakitafuta mbadala wa kocha wao wa sasa, Jupp Heynckes, ambaye anataka kustaafu tena mwishoni mwa msimu tangu arejee kufanya kazi kwa mufda, Oktoba mwaka jana.
    Bayern imethibitisha leo kwamba Kovac, ambaye kwa sasa anaifundisha timu nyingine ya Bundesliga, Frankfurt, amekubali kuwa kocha mpya wa timu hiyo kuanzia msimu ujao hadi mwaka 2021.
    Niko Kovac atachukua nafasi ya Jupp Heynckes Bayern Muchi kuanzia Julai 1, mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 alidumu kwa misimu miwili Bavaria kuanzia mwaka 2001 hadi 2003 ambako alicheza mechi mechi 51 na kuisaidia Bayern kutwaa taji la  Bundesliga na Kombe la Ujerumani.
    Makocha kadhaa wametajwa kuchukua nafasi hiyo itakayoachwa wazi muda si mrefu, akiwemo kocha wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel na wa Paris Saint-Germain, Unai Emery.
    Pamoja na hayo, imekuwa ikiripotiwa kwa mapana marefu nchini Ujerumani kwamba Kovac atachukua nafasi hiyo, habari ambazo zimethibitishwa leo kupitia ukurasa wa Twitter wa klabu hiyo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIKO KOVAC NDIYE KOCHA MPYA BAYERN MUNICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top