• HABARI MPYA

  Sunday, April 15, 2018

  MSUVA AFUNGA MAWILI NA KUINUSURU JADIDA KUCHAPWA UGENINI LIGI YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, KHOURIBGA 
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva leo amefunga mabao mawili timu yake, Difaa Hassan El Jadida ikilazimisha sare ya 3-3 ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco dhidi ya wenyeji, Olympique de Khouribga Uwanja wa Phosphate mjini Khouribga.
  Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Jadida na kushuka kwa nafasi moja hadi ya nne kwenye Ligi ya Morocco yenye timu 16, ikifikisha pointi zake 38 baada ya kucheza mechi 25.
  Msuva amefunga mabao yake dakika za 65 na dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, hilo likiwa bao lililoinusuru Jadidi kupoteza mechi leo na kuibuka shujaa wa timu yake, wakati bao lingine la timu hiyo limefungwa na Tarik Astati dakika ya 33.
  Simon Msuva leo amefunga mabao mawili, Difaa Hassan El Jadida ikilazimisha sare ya 3-3 na Olympique de Khouribga 

  Mabao ya Khouribga yamefungwa na Zouhair El Moutaraji mawili dakika za nne na 38 na Adam Nafati dakika ya 55.
  Kikosi cha Difaa Hassan El-Jadida kilikuwa; Aziz El Qinani, Fabrice Ngah, Youssef Aguerdoum, Tarik Astati, Mohamed Hamami, Bakary N'diaye, Marouane Hadhoudi, Bilal El Magri, Saimon Msuva, Ayoub Nanah na Mario Mandrault Bernard.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AFUNGA MAWILI NA KUINUSURU JADIDA KUCHAPWA UGENINI LIGI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top