• HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2018

    WAMBURA ADAIWA KUGHUSHI BARUA NA KUPOKEA ‘FEDHA HARAMU’ ZA TFF

    KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inakutana leo Machi 14, 2018 pamoja na mambo mengine itajadili suala la Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura (pichani kulia) aliyefikishwa kwenye kamati kwa makosa matatu ya kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kugushi  barua na kushusha hadhi ya TFF.
    Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba, Wambura amefikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.
    Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomuhusu Wambura ikiwa ni uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa mwaka 2015.
    Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili baadaye leo na ana hiyari ya kufika kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo,kutuma kwa maandishi,kuleta mashahidi au kutuma muwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi.
    Makosa anayoshtakiwa Wambura ni; 1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013
    2. Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
    3. Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAMBURA ADAIWA KUGHUSHI BARUA NA KUPOKEA ‘FEDHA HARAMU’ ZA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top