• HABARI MPYA

    Tuesday, March 13, 2018

    TIMU ZA VIJANA; NGORONGORO KUCHEZA NA MOROCCO NA MSUMBIJI, SERENGETI BOYS KUJIANDAA NA CECAFA, U-13 WAENDA UBELGIJI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbuji kabla ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana (AFCON U20).
    Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji Jumatano Machi 21, 2018 michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili jijini Kinshansha Congo DR.
    Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.
    Timu ya Taifa chini ya miaka 16 Serengeti Boys inaendelea kujiandaa na mashindano ya CECAFA kwa vijana yatakayofanyika Burundi.
    Kikosi hicho kipo kambini kwenye hostel za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF,Karume-Ilala,Dar es Salaam.
    Mashindano hayo ya CECAFA kwa Vijana yataanza April 1 mpaka April 15 huko Burundi.
    Wakati huo huo: Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 13 (U13) inatarajiwa kushiriki michuano ya vijana itakayozikutanisha timu za vijana za nchi zaidi ya 10 kutoka mataifa mbalimbali yatakayofanyika nchini Ubelgiji mwezi Agosti, 2018.
    TFF inaandaa utaratibu sahihi wa kupata kikosi cha timu ya Taifa kwa vijana wenye umri huo ili kuweza kujiandaa na michuano hiyo ya vijana.
    Kwa kuanzia kutachezwa mechi kati ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 kutoka Tanzania Bara dhidi ya vijana wa Zanzibar katika siku za hivi karibuni ili kutoa nafasi kwa waalimu kuchaguwa wachezaji wenye vipaji watakaounda kikosi hicho cha U13.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU ZA VIJANA; NGORONGORO KUCHEZA NA MOROCCO NA MSUMBIJI, SERENGETI BOYS KUJIANDAA NA CECAFA, U-13 WAENDA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top