• HABARI MPYA

  Sunday, March 11, 2018

  TANZANIA PRISONS YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-1 NA KUPAA NAFASI YA NNE LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Tanzania Prisons imepanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidiya Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya Jeshi la Magereza ifikishe pointi 36 baada ya kucheza mechi 22 na kusogea nafasi ya nne, ikiishusha Singida United yenye pointi 36 pia za mechi 22, lakini inazidiwa wastani wa mabao.
  Mabao ya Prisons yote yamefungwa na beki Salum KImenya, ambaye leo alichezeshwa kama kiungo mshambuliaji na kuonyesha uwezo mkubwa akitikiwsa nyavu dakika za 45 na 49.
  Bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na mshambuliaji Stahmil Mbonde kwa penalti dakika ya 32, kufuatia kiungo Mohammed Issa ‘Banka’ kuangushwa kwenye boksi.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Mbeya City Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Mabao ya Ruvu yamefungwa na Khamis Mcha 'Vialli' dk61 na Ishara Juma dakika ya 90, wakati ya Mbeya City yamefungwa na Eliud Ambokile dakika ya 13 na Frank Ikobela dakika 53.
  Singida United imelazimishwa sare 0-0 na Ndanda FC Uwanja wa Namfua mjinio Singida na Maji Maji nayo imetoa sare ya 0-0 pia Lipuli FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja, mabingwa watetezi, Yanga wakiwakaribisha Stand United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-1 NA KUPAA NAFASI YA NNE LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top