• HABARI MPYA

    Tuesday, March 13, 2018

    SINGIDA UNITED NA YANGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION APRILI 1

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    ROBO Fainali za michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi Machi katika viwanja vinne tofauti nchini.
    Ijumaa Machi 30, 2018 kutakuwa na mchezo mmoja katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ambapo wenyeji Stand United watawakaribisha Njombe Mji saa 10:00 jioni.
    Machi 31, 2018 kutakuwa na michezo miwili, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania saa 8:00 mchana Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku saa 2:00 usiku Azam FC watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam. 
    Jumapili Aprili Mosi, 2018 kutakuwa na mchezo mmoja, Singida United watakuwa wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Namfua mjini Singida Aprili Mosi, 2018 mchezo utakaonza saa 10:00 jioni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA UNITED NA YANGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION APRILI 1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top