• HABARI MPYA

    Tuesday, March 06, 2018

    SIMBA SC: TUKO TAYARI KUWZIMA AL AMSRY KESHO TAIFA

    Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco amesema kwamba wapo tayari kucheza vizuri na kwa bidii kesho dhidi ya Al Masry ili washinde.
    Simba SC wanawakaribisha Al Masry kesho kuanzia Saa 12:00 jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
    Na kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu, Mfaransa, Pierre Lechantre na Nahodha wa timu, Bocco walijitokeza kuzungumza na Waandishi wa Habari asubuhi ya leo ukumbi wa mikutano ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Katika mkutano huo, kocha Lechantre alisema baada ya maandalizi mazuri, vijana wake wapo tayari kwa mchezo wa kesho.
    Nahodha, Bocco kwa upande wake alisema anafahamu utakuwa mchezo mgumu kwa sababu Al Masry ni timu nzuri kwa rekodi zake na matokeo yake ya nyuma.
    Lakini Bocco akasema hata Simba ni timu nzuri na iona rekodi nzuri pia kwenye michuano ya Afrika, hivyo mchezo wa kesho utakuwa wa ushindani mkubwa.
    Bocco amewaomba wapenzi wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho kuishangilia timu yao ili iweze kupata ushindi nyumbani.   
    Baada ya mchezo wa kesho, timu hizo zitarudiana siku 10 baadaye mjini Cairo, Misri na mshindi wa jumla ataingia kwenye mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi kwa kucheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Timu zinazoingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho hupatiwa dola za Kimarekani 150,000 zaidi ya Sh. Milioni 300 ambazo huongezeka kulingana na matokeo zaidi kuanzia hatua hiyo.
    Bingwa wa Kombe la Shirikisho hupata Dola za Kimarekani 625,000 zaidi ya Sh. Bilioni 1.5, mshindi wa Pili wakati mshindi wa pili wa Kundi hupata dola 239,000 sawa na wa tatu wakati mshindi wa nne hupata dola 150,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC: TUKO TAYARI KUWZIMA AL AMSRY KESHO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top