• HABARI MPYA

    Thursday, March 15, 2018

    SIMBA SC TAYARI WAPO PORT SAID BAADA YA SAFARI NDEFU YA NDEGE NA BASI TANGU JANA

    Na Mwandishi Wetu, CAIRO
    MSAFARA wa Simba SC umewasili salama mjini Port Said majira ya Saa 12 na ushei asubuhi kwa Saa za hapa na saa moja zaidi kwa saa za Afrika Mashariki, tayari kwa mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Al Masry Jumamosi.
    Simba itakuwa ugenini dhidi ya Al Masry katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Port Said mjini Port Said, Misri ikihitaji ushindi wowote kusonga mbele, baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Jumatano wiki iliyopita.
    Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo, Simba SC ikaanza safari ya saa tatu kwa barabara kuja mji wa Port Said kwa basi maalum la kukodi.
    Kikosi cha Simba SC baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo, kabla ya kupanda basi kwend Port Said

    Laudit Mavugo akiwaongoza wenzake baada ya kuwasili mjimi Port Said
    Simba iliwasili Cairo Saa 7:50 usiku wa jana ikitokea Addis Ababa, Ethiopia ambako ilipitia kuunganisha ndege ikitokea Dar es Salaam ambako iliondoka jioni jana.
    Mkuu wa Msafara, James Mhagama ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuwasili hapa alimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Misri, Said Suleim Nassor pamoja na wenyeji wao, Al Masry kwa mapokezi mazuri.
    Msafara wa Simba SC upo chini ya Kaimu Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’ na unaundwa na wachezaji 20, ambao ni makipa; Said Mohamed 'Nduda' na Aishi Manula, mabeki; Yussuf Mlipili, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Mganda Juuko Murushid, Mghana Asante Kwasi, Erasto Nyoni na Paul Bukaba.
    Viungo; Mghana James Kotei, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Shiza Kichuya na washambuliaji ni Mganda Emmanuel Okwi, Mrundi Laudit Mavugo, John Bocco, Mghana Nicholaus Gyan na Juma Luizio.
    Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre, Msaidizi, Mrundi Masoud Juma, Kocha wa Mazoezi ya Nguvu, Mtunisia Mohammed Aymen Hbibi, kocha wa makipa, mzalendo Muharami Mohammed ‘Shilton’,  Dk. Yassin Gembe, Meneja Richard Robert na Mtunza Vifaa Yassin Mtambo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC TAYARI WAPO PORT SAID BAADA YA SAFARI NDEFU YA NDEGE NA BASI TANGU JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top