• HABARI MPYA

  Sunday, March 04, 2018

  SAMATTA ATOKEA BENCHI GENK YASHINDA 1-0 UGENINI UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, BEVERIN
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumamosi ametokea benchi timu yake KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Waasland-Beveren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Freethiel.
  Samatta aliingia dakika ya 70 jana kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis baada ya kukosekana kabisa uwanjani wiki iliyopita, Februari 23, Genk wakishinda 4-0 dhidi ya Antwerp Uwanja wa nyumbani, Luminus Arena kutokana na maumivu ya goti.
  Bao pekee la Genk katika ushindi wa ugenini jana kwenye mchezo huo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, lilifungwa na beki Mgambia, Omar Colley dakika ya 68 akimalizia kazi nzuri ya kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy.
  Samatta jana alicheza mechi ya 77 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
  Kikosi cha Waasland-Beveren kilikuwa; Roef, Demir, Angban/Ndiaye dk83, Jans, Ampomah/Mmae dk80, Caufriez, Myny/Boljevic dk70, Schryvers, Camacho, Thelin na Ait-Atmane.
  KRC Genk: Vukovic, Nastic, Colley, Aidoo, Mata, Wouters/Buffalo dk45, Seck, Malinovskyi, Pozuelo/Uronen dk84, Ndongala na Karelis/Samatta dk70.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI GENK YASHINDA 1-0 UGENINI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top