• HABARI MPYA

  Sunday, March 04, 2018

  RONALDO AFUNGA MAWILI REAL MADRID YASHINDA 3-1 LA LIGA

  Mwanasoka Bora wa Dunia, Mreno Cristiano Ronaldo akinyoosha mkono juu kishujaa baada ya kuifungia Real Madrid mabao mawili dakika za 45 na ushei na 78 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Getafe kwenye mchezo wa La Liga usiku wa Jumamosi Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid. Bao la Kwanza la Real Madrid lilifungwa na Gareth Bale dakika ya 24, wakati la Getafe iliyomaliza pungufu baada ya  Loic Remy kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 47, lilifungwa na Francisco Portillo dakika ya 65.
  Real sasa wanahamishia nguvu zao katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG Jumanne mjini Paris wakitakiwa kwenda kuulinda ushindi wao wa 3-1 ili kwenda Robo Fainali PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AFUNGA MAWILI REAL MADRID YASHINDA 3-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top