• HABARI MPYA

  Sunday, March 11, 2018

  REFA MTUHUMIWA SAKATA LA KUPANGA MAOKEO BURUNDI ASIMAMISHWA ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimemsimamisha refa Mfaume Ali Nassor (pichani kushoto) kwa muda kupisha uchunguzi dhidi yake juu ya tuhuma za rushwa.
  Mfaume, kwa pamoja na marefa wengine watatu wa Tanzania Bara, Frank Komba, Israel Mujuni Nkongo na Sudi Lila wanachunguzwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa tuhuma za upangaji matokeo.
  Timu hiyo ya marefa wa Tanzania ilichezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Lydia Ludic Burundi Academic ya Burundi na Rayon Sports ya Rwanda kati ya Februari 21, mwaka huu mjini Bujumbura.
  Inadaiwa kabla ya mchezo huo ambao Kamisaa alikuwa Gladmore Muzambi wa Zimbabwe, viongozi wa Rayon walikwenda hoteli kukutana na marefa hao wa Tanzania.
  Inadaiwa ushahidi wa picha za kamera CCTV unamuonyesha Ofisa w Rayon akiingia kwenye chumba cha refa wa akina, Nkongo ambaye naye kwa sasa pamoja na wenzake wanachunguzwa na CAF.
  Bado Shirikisho la Soka Tanzania (CAF) halijatoa tamko lolote kuhusu marefa wake wanaochunguzwa, zaidi ya tamko tu kwmaba wamepokea taarifa hiyo na wanaacha uchunguzi uendelee.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA MTUHUMIWA SAKATA LA KUPANGA MAOKEO BURUNDI ASIMAMISHWA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top