• HABARI MPYA

    Wednesday, March 07, 2018

    KARIA AWATUMA SALAMU ZA POLE CYPRUS BAADA YA KIFO CHA RAIS WA FA YAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za pole kwa Chama cha Soka Cyprus kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Rais wa FA ya nchi hiyo, Costakis Koutsokoumnis.
    Rais wa TFF Ndugu Karia amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wakongwe wa mpira wa Miguu.
    “Koutsokoumnis alikuwa muhimiri mkubwa kwa soka la Cyprus na amefariki katika wakati ambao Cyprus na mpira kiujumla ulikuwa unamuhitaji,nimesikitishwa na kifo chake na ninatoa pole kwa familia yake,FA ya  Cyprus,FIFA na familia ya soka kwa ujumla” Alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.
    Wallace Karia (kushoto) ametuma salamu za pole kwa Chama cha Soka Cyprus kufuatia kifo cha Rais wa FA ya nchi hiyo, Costakis Koutsokoumnis

    Hadi umauti unamkuta Koutsokoumnis alikuwa ndio Rais wa FA ya Cyprus na amekuwa kwenye kamati mbalimbali za FIFA akiwa Makamu Mwenyekiti na alianza kutumikia soka la Cyprus tokea mwaka 1990.
    Amewahi kuwa Makamu wa Rais wa FA ya Cyprus kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa FA hiyo mwaka 2001 nafasi aliyoitumikia mpaka mauti yanamkuta.

    Koutsokoumnis amefariki Machi 5, 2018 akiwa na miaka 61 baada ya miezi kadhaa ya kupigana kupona ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KARIA AWATUMA SALAMU ZA POLE CYPRUS BAADA YA KIFO CHA RAIS WA FA YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top