• HABARI MPYA

  Saturday, March 17, 2018

  RAIS WA CAF, AHMAD ATIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI CAF

  RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad wa Madagascar leo ametimiza mwaka mmoja madarakani tangu ashinde nafasi hiyo Machi na kuhitimisha miaka 29 ya utawala wa Mcameroon, Issa Hayatou.
  Katika mwaka wake mmoja madarakani, miongoni mwa mambo yanayohesabiwa kama ni mafanikio ni mabadiliko ya kalenda ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia mwaka 2019, ili kuwapa uhuru wachezaji wanaocheza Ulaya kutoondoka katika klabu zao katikati ya msimu.
  Rais wa CAF, Ahmad (kulia) akiwa na Mtendaji Mkuu wa Bin Zubeiry Sports - Online, Mahmoud Zubeiry (kushoto)

  Kubadilishwa kwa kalenda ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa kutoka Februari na November hadi Septemba na Mei, ili kwenda sabamba na Ligi nyingi za nyumbani za Afrika.
  Aidha, wanawake wawili, Isha Johansen wa Sierra Leone na Lydia Nsekera wa Burundi kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ya CAF inahesabiwa kama mafanikio pia sambamba na shirikisho hilo kuanzisha utaratibu wa kuwalipa marefa wanaopangiwa kiuchezesha mechi za kimataifa badala ya jukumu hilo kupewa nchi au klabu mwenyeji, inayoondoa shinikizo la waamuzi kuzipendelea timu wenyeji.
  Lakini pia changamoto mbalimbali zimeainishwa ikiwemo Cameroon kukimbizana na muda kufanikisha uenyeji wao wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani, 2019, ongezekao na Super Cup ya CAF ambayo bingwa wa Ligi ya Mabingwa ambayo anakuwa mwenyeji wa bingwa wa Kombe la Shirikisho, inastahili kuchezwa nyumbani na ugenini.
  Nyota zaidi wa zamani wa wanepatiwa nafasi CAF, ukiondoa Mwanasoka Bora wa Mwaka 1988, Kalusha Bwalya wa Zambia, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS WA CAF, AHMAD ATIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top