• HABARI MPYA

  Sunday, March 04, 2018

  PRISONS YAZIDI KUJISOGEZA ANGA ZA UBINGWA, YAICHAPA 1-0 MBAO FC

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Tanzania Prisons leo imeichapa bao 1-0 Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Bao pekee katika mchezo huo ulioanza Saa 10:30 jioni, bao pekee la Tanzania Prisons lilifungwa na mshambuliaji wake, Mohammed Rashid kwa penalti dakika ya 11.
  Matokeo hayo yanaifanya Prisons ifikishe pointi 32 baada ya kucheza mechi 20, wakiendelea kukaa nafasi ya tano, nyuma ya Singida United pointi 34, Azam FC pointi 38, Yanga SC pointi 40 na Simba SC pointi 46. Timu zote zimecheza mechi 20, kasoro Yanga 19. 
  Mapema Saa 8:00 mchana ulifanyika mchezo mwingine wa Ligi Kuu, Mbeya City ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mwadui FC ya Shinyanga.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Lipuli imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Samora mjini Iringa. 
  Mabao ya Lipuli yalipatikana dakika ya 19 na 64 yote yakifungwa na Adam Salamba, wakati la Ndanda FC limefungwa na Nassor Kapama dakika ya 21.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAZIDI KUJISOGEZA ANGA ZA UBINGWA, YAICHAPA 1-0 MBAO FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top