• HABARI MPYA

  Saturday, March 17, 2018

  NGORONGORO NA MOROCCO YAAHIRISHWA HADI KESHO KUPISHA MECHI A SIMBA NA YANGA KWENYE TV

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kirafiki baina timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes na vijana wenzao wa Morocco ulioapangwa kufanyika leo Saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam umeahirshwa hadi kesho.
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamua kuusogeza mchezo huo mbele kwa siku moja ili kuwapa fursa Watanzania wengi kufuatilia mechi za marudiano za hatua ya 32 Bora michuano ya klabu Afrika kwenye Televisheni leo, timu za Simba na Yanga zikiwa ugenini. 
  Simba watakuwa mjini Port Said nchini Misri kumenyana na wenyeji, Al Masry baada ya sare ya 2-2 Jumatano iliyopita Dar es Salaam na Yanga watakuwa mjini Gaborone nchini Botswana kumenyana na wenyeji, Township Rolleres. 
  Katika mchezo wa Ngongoro na Morocco, watazamaji wataingia bure ili kuwapa hamasa Ngorongoro Heroes wawafuge vijana wenzao wa Morocco.
  Ngorongoro iliyo chini ya kocha Ammy Ninje, itakuwa na mechi mbili za kirafiki na mbali na hiyo ya kesho, nyingine itafuatia Jumatano ya Machi 21, dhidi ya Msumbiji.
  Kwa Ngorongoro mechi hizo ni maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ta Afrika (AFCON U20) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Machi 31 Uwanja wa Taifa na marudiano wiki mbili baadaye mjini Kinshasa.
  Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.
  Ninje anapewa Ngorongoro baada ya kuweka rekodi mbaya kwenye Challenge nchini Kenya mwaka jana, Kili Stars ikiondoka bila kushinda hata mechi moja, ikiambulia sare moja na kufungwa mechi zote. Katika michuano hiyo, pamoja na Ninje kuboronga, aliwakera Watanzania kwa majibu yake.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO NA MOROCCO YAAHIRISHWA HADI KESHO KUPISHA MECHI A SIMBA NA YANGA KWENYE TV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top