• HABARI MPYA

  Saturday, March 03, 2018

  NEYMAR AWASILI BELO HORIZONTE KWA AJILI YA UPASUAJI

  NYOTA wa Paris Saint-GermainNeymar amewasili mjini Belo Horizonte akiwa na mama yake, Nadine Goncalves Da Silva and na Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar jana tayari kwa upasuaji wa mguu.
  Nyota huyo wa anatarajiwa kufanyiwaupasuaji wa mguu baada ya kuumia enka Jumamosi iliyopita, timu yake PSG ikishinda 3-0 katika Ligi ya Ufaransa, Ligue 1 dhidi ya Marseille.
  Pamoja na klabu yake awali kusema mchezaji huyo hakuhitaji upasuaji, lakini mshambuliaji huyo jana usiku aliwasili katika hospitali ya Mater Dei Hospitalhuyo nchini kwao, Brazil.
  Neymar amewasili na Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar mjini Belo Horizonte jana usiku PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Brazil imeamua kumchukua Neymar kumtibu haraka ili isije ikamkosa kwenye Fainali za kombe la Dunia nchini Urusi katikati ya mwaka. 
  Sasa PSG wanaelekea kwenye mchezo wa marudiano wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki ijayo bila Neymar wakitakiwa kuifunga Real Madrid 2-0 mjini Paris ili kwenda Robo Fainali, kufuatia kufungwa 3-1 kwenye mchezo wa kwanza Madrid.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR AWASILI BELO HORIZONTE KWA AJILI YA UPASUAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top