• HABARI MPYA

    Saturday, March 03, 2018

    MTOTO WA RAIS WEAH AULA PSG KUELEKEA MECHI NA REAL MADRID

    KINDA Timothy Weah, mtoto gwiji wa Paris Saint-Germain na mshindi wa zamani wa Ballon d'Or, George, amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 na kocha Unai Emery kuelekea mechi ijayo ya Ligue 1 dhidi ya Troyes.
    Vinara hao wa Ligue 1 wanakabiliwa na mapungufu katika safu yao ya ushambuliaji kufuatia kuumia kwa Neymar, huku pia Kylian Mbappe na Edinson Cavani wote wakiondolewa kwenye kikosi cha kucheza dhidi ya Troyes.

    Timothy Weah amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 cha PSG kitakachoivaa Troyes leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Kocha Emery anahofia nyota wake hao wanaweza kuumia kuelekea mechi muhimu ya marudiano ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. 
    Kinda huyo wa umri wa miaka 18 anafuata nyayo za baba yake ambaye kwa sasa ni Rais wa Liberia ambaye enzi zake alichezea PSG kwa miaka mitatu na kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mwaka 1995 kabla ya kuhamia AC Milan. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTOTO WA RAIS WEAH AULA PSG KUELEKEA MECHI NA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top