• HABARI MPYA

  Friday, March 09, 2018

  MILIONI 56 ZAPATIKANA MECHI YA YANGA NA TOWNSHIP ROLLERS JUMANNE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga SC na Township Rollers ya Botswana uliochezwa Jumanne wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam umeingiza jumla ya Sh 56,245,000.
  Kiasi hicho cha fedha kimetokana na jumla ya watazamaji 9,961 waliojitokeza kuushuhudia mchezo huo ambao wenyeji, Yanga SC walichapwa mabao 2-1.
  Katika mashabiki hao 9,961 ni 99 tu walioketi jukwaa la VIP A ambako kiingilio kilikuwa Sh 20,000 na kupatikana jumla ya Sh. 1,980,000 na 991 waliketi VIP B na C kwa kiingilio cha shilingi 10,000 ambako ilipatikana Sh. 9,910,000.
  Mechi ya Yanga SC na Township Rollers ya Botswana imeingiza Sh Milioni 56 

  Katika majukwa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani ndiko waliketi watazamaji wengi zaidi 8,871 kwa kiingilio ncha shilingi 5,000 na zimepatikana jumla ya Sh. 44,355,000
  Katika fedha hizo, Sh. zimekatwa kodi ya VAT Sh. 8,579,745.76, Selcom Sh. 3,318,455.00, TFF Sh. 2,217,339.96, Uwanja  6,652,019.89, Gharama za mchezo Sh. 3,991,211.93, BMT Sh. 443,467.99, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepelekewa Sh. 2,217,339.96 na klabu yenyewe, Yanga SC imepata Sh. 28,825,419.50
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MILIONI 56 ZAPATIKANA MECHI YA YANGA NA TOWNSHIP ROLLERS JUMANNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top