• HABARI MPYA

  Saturday, March 03, 2018

  MECHI YA SIMBA NA EL-MASRY SASA KUCHEZWA USIKU JUMATANO UWANJA WA TAIFA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  MECHI ya kwanza ya Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Simba SC na El-Masry ya Misri iliyopangwa kufanyika Jumatano ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imesogezwa hadi Saa 12:00 kutoka Saa 10:00 jioni.
  Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara katika mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam leo.
  Manara amesema kwamba wameisogeza mbele mechi hiyo kwa sababu Jumatano ni siku ya kazi na wamefanya hivyo ili kuwapa fursa mashabiki na wapenzi wengi zaidi wa Simba kujitokeza uwanjani baada ya kumaliza pilika zao za kutwa za kujitafutia riziki.
  Emmanuel Okwi (kulia) na Nahodha John Bocco (kushoto) wote wapo fiti kuelekea mechi na El Masry Jumatano

  Manara mtoto wa gwiji wa klabu ya Yanga, Sunday Manara amezungumzia pia maandalizi ya mchezo huo akisema yamekamilika na El-Masry wanatarajiwa kuwasili kesho kabla ya kufanya mazoezi Jumanne Uwanja wa Taifa.
  Amesema Simba ipo kambini kwenye hoteli ya SeaScape, Kunduchi mjini Dar es Salaam tang utu baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana wakilazimishwa sare ya 3-3 na Stand United Uwanja wa Taifa.
  Kuhusu washambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na Nahodha John Bocco ambao walikosekana jana wote kwa sababu ya maumivu, Manara amesema wanaendelea vizuri pamoja na Mnyarwanda, kiungo Haruna Niyonzima aliyekuwa India kwa matibabu.
  “Kwa upande wa wachezaji wetu ambao ni majeruhi Haruna amekwisharudi kutoka India alipokwenda kwa ajili ya matibabu na ametibiwa na ndani ya hizi siku mbili atajiunga na kikosi, kwa upande wa Bocco na Okwi wapo salama na tuliona tuwapumzishe,"amesema Haji.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA SIMBA NA EL-MASRY SASA KUCHEZWA USIKU JUMATANO UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top