• HABARI MPYA

  Tuesday, March 13, 2018

  LWANDAMINA APANIA KUFANYA MAAJABU BOTSWANA, ASEMA VIJANA WAKE WAPO KIKAZI ZAIDI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba vijana wake wamejipanga kuhakikisha wanashinda mechi ya marudiano na Township Rollers nchini Botswana na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Baada ya kufungwa mabao 2-1 wiki iliyopita katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga inatakiwa kushinda 2-0 mjini Gaborone Jumamosi ili kwenda hatua ya makundi.
  Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 10, wakiwemo wanane wa benchi la Ufundi kimeondoka Alfajiri ya leo kwa ndege kwenda Gaborone, wachezaji wakiwa na ari kubwa baada ya ushindi wa 3-1 jana dhidi ya Stand United ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Taifa.
  Kocha wa Yanga SC, George Lwandamina amesema wamejipanga kushinda mechi ya marudiano na Township Rollers nchini Botswana  

  Na wakati wa safari Lwandamina amesema kwamba hajakata tamaa kwa matokeo ya kufungwa nyumbani, kwani anaamini hata vijana wake wanaweza kwenda kushinda ugenini pia. 
  “Kwenye mpira kila kitu kinawezekana, nina matumaini makubwa ya kufanya vizuri ugenini, kutokana na morali  ya vijana wangu ” alisema Lwandamina.
  Wachezaji wa Yanga SC walioondoka leo ni pamoja na makipa; Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, mabeki Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Pato Ngonyani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani.
  Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Yussuf Mhilu, Pius Buswita, Obrey Chirwa, Raphael Daudi, Juma Mahadhi, Ibrahim Ajib, Thabani Kamusoko, Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya.
  Upande wa viongozi ni pamoja na kocha Mkuu, Lwandamina, wasaidizi wake Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazalendo Nsajigwa Shadrack, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli Jacob Onyango na Meneja Hafidh Saleh wakati viongozi ni Omar Kaaya, Samuel Lukumay na Elias Mwanjala. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA APANIA KUFANYA MAAJABU BOTSWANA, ASEMA VIJANA WAKE WAPO KIKAZI ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top