• HABARI MPYA

  Friday, March 16, 2018

  ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA 2018 HATARI TUPU

  Taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya limeonyeshwa leo wakati droo iliyofanyika makao makuu ya UEFA mjini Nyon, Uswisi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  RATIBA ROBO FAIBALI LIGI YA MABINGWA

  Barcelona vs Roma
  Sevilla vs Bayern Munich
  Juventus vs Real Madrid
  Liverpool vs Manchester City 
  Mechi za kwanza zitachezwa Aprili 3-4
  Mechi za marudiano zitachezwa Aprili 10-11 
  TIMU za England, Liverpool na Manchester City zitamenyana zenyewe kwa zenyewe katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya .
  Katika droo iliyofanyika makao makuu ya UEFA mjini Nyon, Uswisi, timu hizo zitakutana katika mchezo wa kwanza utakaofanyika Uwanja wa Anfield kabla ya kurudiana Uwanja wa Etihad.
  Timu zote tatu za Hispania zimetanganishwa katika hatua hii, Barcelona wakimenyana na Roma, Real Madrid wakicheza na Juventus katika marudio ya fainali ya mwaka jana wakati Sevilla imepewa Bayern Munich.
  Manchester City walitinga hatua hii ya pili ya mtoano kwa ushindi wa jumla wa 5-2 dhidi ya mabingwa wa Uswisi, Basle, lakini kipigo cha nyumbani katika mchezo wa marudiao kinapaswa kumuamsha kocha Pep Guardiola.
  Mspaniola huyo bado anapewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo kubwa la Ulaya mbele ya vigogo wa Hispania, Barcelona na Real Madrid ambao wote wamewatoa wapinzani wagumu kufika hatua hii.
  Real Madrid wamewatoa Paris Saint-Germain ya Ufaransa iliyokuwa pia inapewa nafasi kubwa ya kushinda taji hili, shukrani kwake Cristiano Ronaldo aliyeonyesha kiwango kizuri kwenye mechi zote mbili.
  Mreno huyo, Mwanasoka bora wa Dunia alifunga mabao matatu kikosi cha Zinedine Zidane kikipata ushindi wa jumla wa 5-2.
  Barcelona ilionja ushindani wa Ligi Kuu ya England kwa kuwang'oa Chelsea, wakati Sevilla iliitoa Manchester United ya Jose Mourinho kwa kuifunga Uwanja wa Old Trafford 2-1 baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza Hispania.
  Pamoja na upangaji wa ratiba ya Robo Fainali, pia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya lilionyeshwa leo katika droo iliyofanyika makao makuu ya UEFA mjini Nyon, Uswisi
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA 2018 HATARI TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top