• HABARI MPYA

  Saturday, March 17, 2018

  KILA LA HERI SIMBA NA YANGA MISRI NA BOTSWANA LEO…TUNAWATAKIA USHINDI NA KUSONGA MBELE

  WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Afrika, Simba na Yanga leo wapo ugenini kwa michezo ya marudiano ya hatua ya 32 Bora.
  Yanga watakuwa wageni wa Township Rollers Uwanja wa Taifa mjini Gaborone, Botswana kuanzia Saa 10:45 jioni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa na Simba watakuwa wageni wa Al Masry Uwanja wa Port Said nchini Misri kuanzia Saa 2:30 usiku.
  Yanga wanahitaji lazima ushindi wa mabao 2-0 ili kwenda hatua ya makundi, baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumanne ya wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Simba SC wanataka ushindi wowote, hata wa 1-0 ili kusonga mbele katika hatua ya mwisho ya mchujo baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
  Yanga ikiitoa Rollers itakwenda hatua ta makundi ya Ligi ya Mabingwa, ambayo kihistoria itakuwa mara yake ya pili baada ya mwaka 1998, lakini tolewa itaingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
  Simba SC ikishinda leo itacheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho, lakini ikitolewa itarejea nyumbani moja kwa moja.
  Kila la heri wawakilishi wetu. Mungu zibariki Simba na Yanga. Mungu ibariki Tanzania. Amin.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILA LA HERI SIMBA NA YANGA MISRI NA BOTSWANA LEO…TUNAWATAKIA USHINDI NA KUSONGA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top