• HABARI MPYA

    Monday, March 05, 2018

    KAMUSOKO ALIVYOJIFUA NA YANGA KIKAMILIFU LEO GYMKHANA KUELEKEA MECHI YA KESHO

    Kiungo aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, Mzimbabwe Thabani Kamusoko akitafuta maarifa ya kuchukua mpira kwa Ibrahim Ajib (kushoto) wakati wa mazoezi ya Yanga SC leo jioni Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 
    Kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi akiudhibiti mpira mbele ya Nahodha na beki Mzanzibari, Nadir Haroub 'Cannavaro' 
    Juma Mahadhi (katikati) aliyekuwa mgonjwa pia naye amefanya mazoezi kikamilifu leo
    Kushoto ni beki tegemeo, Kevin Yondan akiwa mazoezini na wenzake 
    Beki Abdallah Hajji 'Ninja' (wa tatu kulia) aliyekuwa majeruhi pia, naye amefanya mazoezi leo  
    Kipa Mcameroon Youthe Rostand amefanya mazoezi pia kuelekea mchezo wa kesho
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMUSOKO ALIVYOJIFUA NA YANGA KIKAMILIFU LEO GYMKHANA KUELEKEA MECHI YA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top