• HABARI MPYA

  Saturday, March 03, 2018

  KAGERA SUGAR YAIBAMIZA MAJI MAJI 2-1 KAITABA, MVUA YAILAZA MECHI YA PRISONS NA MBAO

  Na Mwandishi Wetu, KAGERA
  TIMU ya Kagera Sugar imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Maji Maji ya Songea katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jioni ya leo.
  Hadi mapumziko, Kagera Sugar walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliajiwa zamani wa Simba SC, Christopher Edward Shijja dakika ya 35.
  Na dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerson ‘Jerry’ ’John Tegete akaisawazishia Maji Maji. 
  Christopher Edward akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Kagera Sugar leo

  Wenyeji, Kagera Sugar wakafunguka kufanya mashambulizi ya nguvu kusaka bao lwa kusawazisha na wakafanikiwa dakika ya 72 kufunga la pili kupitia kwa Japhet Makalai.
  Matokeo hayo yanairudisha Maji Maji nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, mbele ya Njombe Mji zote zote zikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 20, wakati Maji Maji sasa ndiyo inashika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 20 pia.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu kati ya wenyeji, Tanzania Prisons na Mbao FC ya Mwanza imeahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Mbeya leo.

  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAIBAMIZA MAJI MAJI 2-1 KAITABA, MVUA YAILAZA MECHI YA PRISONS NA MBAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top