• HABARI MPYA

  Wednesday, March 14, 2018

  KAGERA SUGAR YAFUFUA MATUMAINI YA KUBAKI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Kagera Sugar imefanikiwa kujiondoa kwenye eneo la hatari la kushuka Daraja baada ya ushindi wa 1-0 jana dhidi ya Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Asante kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, Japeh Makalai dakika ya 26 na sasa Kagera Sugar inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 22, ikipanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya 12, ikiiteremshia nafasi ya 13 Mwadui FC.
  Maji Maji ya Songea kwa sasa ndiyo inashika mkia ikiwa na pointi zake 16 za mechi 22, nyuma ya Njombe Mji FC pointi 18 mechi 21, Mbao FC pointi 19 mechi 22 na Mwadui. 
  Lakini bado pointi 21 haziiweki salama sana Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime, kwani Njombe Mji FC wana mchezo mmoja wa kiporo dhidi ya Simba SC ulioahirishwa mwishoni mwa wiki.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAFUFUA MATUMAINI YA KUBAKI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top