• HABARI MPYA

    Friday, March 09, 2018

    KAGERA SUGAR NA MWADUI SASA KUPIGWA JUMATATU KAITABA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
    MZUNGUKO wa 22 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaendelea wikiendi hii Machi 11, 2018 kwa kuchezwa mechi tano (5)
    Mechi mbili za mzunguko huo zilizokuwa zichezwe Machi 11, 2018 zimebadilishiwa tarehe.
    Simba waliokuwa wacheze ugenini dhidi ya Njombe Mji mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine baada ya Simba kuomba kusogezwa kwa mchezo huo ili kupata muda wa maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utakaochezwa Port Said nchini Misri Machi 17, 2018.
    Mchezo wa Kagera na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11, 2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne Machi 13, 2018 kutokana na kusogezwa kwa mchezo wao dhidi ya Yanga SC unaochezwa leo Machi 9, 2018.
    Mechi nyingine za mzunguko wa 22 zitakazochezwa Jumapili Machi 11, 2018; AzamFC  na Mbao FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam na Ruvu Shooting na Mbeya City  Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
    Mechi nyingine za Machi 11 ni Singida United dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Namfua, Maji Maji na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Maji Maji na Tanzania Prisons dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR NA MWADUI SASA KUPIGWA JUMATATU KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top