• HABARI MPYA

  Friday, March 16, 2018

  BORUSSIA DORTMUND, LYON ZANG'OLEWA EUROPA LEAGUE

  TIMU za Borussia Dortmund na Lyon zimetolewa kwenye michuano ya Europa League usiku wa Alhamisi huku ratiba ya Robo Fainali ikitarajiwa kupangwa leo mchana.
  Marseille, Lazio, Salzburg, CSKA Moscow, Sporting Lisbon na Leipzig zinaungana na wapewa nafasi kubwa kubeba taji Atletico Madrid na Arsenal kukamilisha Nane Bora za Europa League 2018.
  Dortmund, mmoja wa mabingwa wa zamani wa Ulaya jana ililazimishwa sare ya 0-0 na Salzburg na kufanya watolewe kwa jumla ya mabao 2-1 waliyofungwa nyumbani.

  Wachezaji wa Borussia Dortmund wakiwa wanyonge jana baada ya kutolewa Europa League
   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  TIMU ZILIZOINGIA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

  Atletico Madrid
  Arsenal
  CSKA Moscow
  Lazio
  Leipzig
  Marseille
  Salzburg
  Sporting Lisbon
  Droo itafanyika mjini Nyon Saa 7:00 mchana leo
  Atletico Madrid itakuwa timu pekee kjuiwakilisha Hispania katika Nane Bora baada ya Athletic Bilbao kufungwa 2-1 nhyumbani na Marseille, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 5-2.
  Lazio walionekana kuingia kwenye mtihani mgumu baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Dynamo Kiev kwenye mchezo wa kwanza, lakini mabao ya kiungo wa zamani wa Liverpool, Lucas na Stefan de Vrij yaliwapa ushindi wa 2-0.
  Salzburg wakaendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika mechi ya 19 na kuwa timu ya kwanza ya Austria kufika Robo Fainali ya Europa League.
  Droo ya leo inaweza kuwakutanisha na RB Leipzig, klabu ya Bundesliga yenye mdhamini mmoja na wao.
  Leipzig imeingia Robo Fainali baada ya sare ya 1-1 na mabingwa wa mwaka 2008 Kombe la UEFA, Zenit St Petersburg na kufanya ushindi wa jumla wa 3-2.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BORUSSIA DORTMUND, LYON ZANG'OLEWA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top