• HABARI MPYA

  Tuesday, March 13, 2018

  BEKI SIMBA APATA AJALI YA PIKIPIKI, AENGULIWA SAFARI YA MISRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AJIALI ya bodabda imemuondoa kikosini beki wa Simba, Salim Mbonde baada ya kuondolewa katika kikosi kinachosafiri nchini kesho kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry, Kombe la Shrikisho Afrika.
  Simba itakuwa ugenini dhidi ya Al Masry katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Port Said mjini Port Said, Misri ikihitaji ushindi wowote kusonga mbele, baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Jumatano wiki iliyopita.
  Beki huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji walikuwepo katika mipango ya Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre kumtumia katika mchezo huo kutokana na ajali hiyo iliyosababisha ashonwe nyuzi tatu juu kidogo ya jicho, amemuondoa katika mipango hiyo.
  Salim Mbonde ameondolewa katika saairi ya Misri kesho baada ya ajali ya pikipiki

  Mbonde alisema hatakuwepo katika mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata katika ajari hiyo kwa kusababisha kushindwa kuendelea na mazoezi ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao.
  “Sitakuwepo katika msafara huo, suala la kuanza lini mazoezi bado sijajua kwani bado sijatoa nyuzi nadhani baada ya kurejea nitaungana na wenzangu baada ya kupata taarifa kutoka kwa daktari wa timu,” alisema Mbonde.
  Beki huyo wa kati, amekutana na majanga hayo baada ya kutoka katika majeruhi yaliyomuweka nje tangu Oktoba 15 mwaka jana alipoumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya timu yake ya zamani, Mtibwa Sugar.
  Kwa ujumla, Simba inawakosa mabeki wake wa kati waliounda ukuta imara mwanzoni mwa msimu, baada ya dirisha dogo pia kumuacha aliyekuwa Nahodha wake, Mzimbabwe, Method Mwanjali aliyekuwa anacheza pamoja na Mbonde.
  Kwa sasa safu ya ulinzi ya Simba iliyopwaya inaundwa na chipukizi Yussuph Mlipili akishirikiana na ama na Erasto Nyoni, James Kotei au Juuko Murshid wakati mwingine – haina watu maalum bado.
  Kikosi cha Simba kinaondoka kesho jioni kwa ndege ya shirika la Ethiopia, msafara ukiongozwa na Kaimu Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’.
  Makipa; Said Mohamed 'Nduda' na Aishi Manula, mabeki; Yussuf Mlipili, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Asante Kwasi, Erasto Nyoni na Paul Bukaba.
  Viungo; James Kotei, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Shiza Kichuya.
  Washambuliaji; Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo, John Bocco, Nicholaus Gyan na Juma Luizio.
  Kocha Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre, Msaidizi, Mrundi Masoud Juma, Kocha wa Mazoezi ya Nguvu, Mtunisia Mohammed Aymen, kocha wa makipa, mzalendo Muharami Mohammed ‘Shilton’,  Dk. Yassin Gembe, Meneja Richard Robert na Mtunza Vifaa Yassin Mtambo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI SIMBA APATA AJALI YA PIKIPIKI, AENGULIWA SAFARI YA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top