• HABARI MPYA

  Tuesday, March 13, 2018

  BEKI MZANZIBAR WA STAND UNITED AZIGOMBANISHA AZAM, SIMBA NA YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kuonyesha kiwango kizuri, beki wa Stand United, Ally Ally ameingia katika rada za timu kubwa hapa nchini Simba, Yanga na Azam FC kuhakikisha wanapata huduma yake kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Beki huyo ameonyesha kiwango kizuri katika mechi mbili alizocheza Dar es Salaam dhidi ya vigogo wa soka nchini, licha ya timu yake kuruhusu mabao sita katika sare ya 3-3 na Simba na kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga.
  Bin Zubeiry Sports - Online lilishuhudia vigogo wa timu hizo tatu, zikimwagia sifa beki huyo jana katika Uwanja wa Taifa, Yanga ilipowakaribisha Stand kwa kusema beki huyo huenda msimu ujao akatua mmoja ya timu hizo kubwa.
  Ally Ally wa Stand United (kushoto) akiwania mpira dhidi ya Mrundi, Laudit Mavugo wa Simba SC

  Walisema kulingana na ubora wake wa kucheza na kuokoa mipira ya vichwa, imewavutia vigogo hao na kudai kwamba mwenye kisu kikali huenda akampata beki huyo.

  Beki huyo alisema hawezi kuzungumzia suala la kuondoka katika timu hiyo kutokana na kubanwa na mkataba wake na timu yake hiyo ya sasa.
  “Bado nina mkataba na Stand, siwezi kuzungumzia kama nipo tayari kuungana na mmoja ya timu hizo, kama wananihitaji wafuate uongozi,” alisema.
  Wakati huo huo, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Athuman Bilal alisema wapo tayari kumruhusu beki huyo hujiunga na timu yoyote kama watafika bei nzuri na maelewano na uongozi wa Stand.
  “Ally ni mchezaji mzuri pia umri wake unaruhusu, lakini bado anamkataba wa miaka mitatu na Stand, kama kuna timu ina hitaji huduma yake benchi la ufundi halina uwezo wa kumzuia,” alisema.
  Bilal alisema hawawezi kuzuia kama anahitaji huduma ya mchezaji huyo, wafuate sheria na kanuni za mchezaji mwenye mkataba anatakiwa kuzungumza na uongozi unayemilika kama ilivyo kwa Ally.
  “Milango ipo wazi waje, uongozi hawawezi kumzuia kwani kinachohitajika na makubaliano ya pande zote mbili, nina imani kuondoka kwake kutapatikana wengine kuziba nafasi yake kutokana na hapa kwetu ni chuo,” alisema Bilal.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI MZANZIBAR WA STAND UNITED AZIGOMBANISHA AZAM, SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top