• HABARI MPYA

  Thursday, March 08, 2018

  AZAM FC YAREJEA NAFASI YA PILI BAADA YA KUIPIGA MWADUI 1-0 CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la mshambuliaji kinda, Yahya Zayed dakika ya tano, limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC ya kocha Mromania Aristica Cioaba inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya pili, mbele ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 40 za mechi 19.
  Yanga inaweza kurudi nafasi ya pili kama itashinda dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Lipuli FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Njombe Mji FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Mabao ya Lipuli yamefungwa na Jerome Lambele dakika ya nane na Adam Salamba dakika ya 77, huku David Obash akiifungia Njombe Mji dakika ya 33.
  Stand United imelazimishwa sare ya 0-0 na Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, wakati bao pekee la John George limeipa ushindi wa 1-0 Ndanda FC dhidi ya Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAREJEA NAFASI YA PILI BAADA YA KUIPIGA MWADUI 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top