• HABARI MPYA

  Thursday, February 08, 2018

  AZAM FC NA KMC...YANGA WAPELEKWA SONGEA KWA MAJI MAJI KOMBE LA TFF

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC itamenyana na KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam, katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Februari 22 na 25 mwaka huu
  Yanga SC watasafiri tena hadi mjini Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Maji Maji.
  Katika droo iliyopangwa jana studio za Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam, mechi zote za hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zitafanyika kati ya Februari 22 na 25.
  Na mbali na Yanga kwenda Songea, vigogo wengine Azam FC watamenyana na KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam, wakati mkoa wa Shinyanga utahodhi mechi mbili mfululizo, kwanza ni Stand United na Dodoma FC na baadaye Buseresere na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kahama.
  Azam FC itamenyana na KMC ya Kinondoni katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya ASFC mjini Dar es Salaam

  Mechi nyingine za hatua hii ni; JKT Tanzania watakuwa wenyeji Ndanda FC Uwanja wa Mbweni, Dar es Salaam, Kiluvya United na Tanzania Prisons Uwanja wa Filbert Bayi, Kibaha, Pwani, Singida United na Polisi Tanzania Uwanja wa Namfua na Njombe Mji dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Saba Saba, Njombe. 
  Ikumbukwe, mabingwa watetezi wa michuano hii, Simba walitolewa katika hatua ya 64 Bora tu kwa mikwaju ya penalti na Green Warriors ya Daraja la Pili baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Warriors nao safari yao ilihitimishwa kwa matuta pia na Singida United pale pae Chamazi katika hatua iliyopita ya 32 Bora.
  Ikumbukwe, vigogo weninge Yanga SC waliponea chupuchupu kuwafuata ‘Wahenga wenzao’, Simba SC baada ya kusawazisha bao dakika ya mwisho kwa penalti ya Obrey Chirwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kupata sare ya 1-1 na Ihefu ya Daraja la pili kabla ya kwenda kusonga mbele kwa penalti pia.
  Na kihistoria Uwanja wa Maji Maji mjini Songea umekuwa mgumu mno kwa Yanga kushinda na mara nyingi matokeo yao mazuri yamekuwa sare katika mechi za Ligi Kuu – na sasa wanakutana katika mechi ya mtoano. Itakuwa shughuli pevu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC NA KMC...YANGA WAPELEKWA SONGEA KWA MAJI MAJI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top