• HABARI MPYA

  Saturday, February 10, 2018

  YANGA SC YAANZA MAWINDO YA TAJI LA LIGI YA MABINGWA, YAFUNGUA DIMBA NA ST LOUIS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC leo wanatupa kete yao ya kwanza katika michuano ya Ligi Mabingwa Afrika watakapomenyana na Saint Louis Suns United ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Yanga SC ya kocha George Lwandamina anayesaidiwa na Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazalendo, Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali, kocha wa makipa inahitaji mtaji wa matokeo mazuri leo kuelekea mechi ya marudiano.
  Habari njema wa wana Yanga ni kwamba, wachezaji wanne kati ya 11 waliokuwa majeruhi leo wamefanya mazoezi kikamilifu.
  Hao ni kipa Youthe Rostand, beki Juma Abdil na viugno Thabani Kamusoko na Ibrahim Hajib ambap wote wamefanya mazoezi kikamilifu na wenzao siku mbili kuelekea mechi hiyo. 
  Aidha, mabeki wazawa Pato Ngonyani na Andrew Vincent ‘Dante’ nao wameanza mazoezi mepesi peke yao, kuashiria wanaweza kurudi kwa ajili ya mchezo wa marudiano wiki mbili baadaye.
  Majeruhi wengine Yanga ni mabeki Mwinyi Hajji Mngwali, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na washambuliaji Yohana Oscar Nkomola, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
  Saint Louis Suns United, inayotokea mji wa Victoria ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa ni muungano wa timu za Saint-Louis iliyoanzishwa mwaka 1985 na Sunshine iliyoanzishwa mwaka 1993.
  Saint Louis ilishinda mataji 13 ya Ligi Daraja la Kwanza Shelisheli kati ya mwaka 1979 na 1994 na imeshiriki michuano ya Afrika mara kadhaa.
  Sunshine kwa upande wake walitwaa taji lao la kwanza mwaka 1995, miaka miwili tu tangu kuanzishwa kwake na mwaka uliofuata Sunshine ilicheza kwa mara ya kwanza michuano ya Afrika.
  Wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye michuano hiyo, Zimamoto ya Zanzibar ambayo leo inaikaribisha Wolaitta Dicha wa Ethiopia Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA MAWINDO YA TAJI LA LIGI YA MABINGWA, YAFUNGUA DIMBA NA ST LOUIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top