• HABARI MPYA

  Saturday, February 03, 2018

  YANGA SC ILIISHINDWA LIPULI DAR NDIYO ITAIWEZA LEO IRINGA?

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  DURU la pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linatarajiwa kuanza leo kwa mechi tano kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini – macho na masikio ya wengie yakielekezwa Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Huko ndiko walipo mabingwa watetezi, Yanga SC ambao watamenyana na wenyeji, Lipuli waliopanda msimu huu kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Mechi ya kwanza ya msimu kati ya Yanga na Lipuli ilimalizika kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Swali ambalo wengi wanajiuliza kuelekea mchezo wa leo Uwanja wa Samora, Yanga ilishindwa kuifunga Lipuli Dar es Salaam, je itaweza leo huko Iringa?  
  Lipuli FC walilazimisha sare ya 1-1 na Yanga SC Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, vipi leo Samora mjini Iringa?
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Azam FC wataikaribisha Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam, Uwanja wa Namfua, Singida United wataikaribisha Mwadui FC ya Shinyanga, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Njombe Mji FC na Songea ni Maji Maji na Mbeya City.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja tu kati ya Simba SC na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Jumatatu kutakuwa na mechi mbili za kukamilisha mzunguko a 16; Stand United na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kambarage na Mbao FC na Kagera Sugar ya Bukoba.
  Februari 8, Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlanduzi mkoni Pwani na Februari 12, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Ikumbukwe ni Simba SC wanaongoza ligi hiyo kwa pointi zao 35, wakifuatiwa na Azam FC pointi 30, Yanga SC pointi 28, Singida United 27 na Mtibwa Sugar 26 baada ya timu zite kucheza mechi 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC ILIISHINDWA LIPULI DAR NDIYO ITAIWEZA LEO IRINGA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top