• HABARI MPYA

  Monday, February 05, 2018

  TIMU YA SAMATTA YAREJEA LIGI KUU, FRIENDS RANGERS HAIKUWA BAHATI YAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya African Lyon imekamilisha idadi ya timu za kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Kiluvya United Uwanja wa Filbert Bayi, Kibaha mkoani Pwani.
  Shukrani kwake Kassim Mdoe mfungaji wa bao pekee la African Lyon, inayomilikiwa na Rahim Kangezi ‘Zamunda’ na kuiwezesha timu yake kuipiku Friends Rangers katika nafasi ya pili ya Kundi A.
  Ikumbukwe katika Kundi A, tayari JKT Tanzania, zamani JKT Ruvu ilikwishapanda na kuziachia kimbembe African Lyon na Friends Rangers kugombea nafasi ya mwisho kupanda kutoka kundi hilo.
  Kikosi cha African Lyon kilichoshuka daraja baada ya msimu wa 2016-2017

  JKT Tanzania nayo leo imeshinda 3-0 dhidi ya Mshikamano FC, Friends Rangers imeshinda 3-1 dhidi ya Mvuvumwa United na Ashanti United imeshinda 3-2 dhidi ya JKT Mgambo.
  Matokeo hayo yanaifanya JKT Tanzania imalize na pointi 37, ikifuatiwa na timu ya zamani ya mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta, Lyon inayofikisha pointi 27, wakati Rangers imemaliza na pointi 25.
  JKT na Lyon zinaungana na Biashara United ya Mara na Alliance Schools ya Mwanza kutoka Kundi B na KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga kutoka Kundi C kukamilisha timu sita za kupanda msimu ujao wa Ligi Kuu.
  Timu mbili zitashuka daraja mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu ili kupata timu 20 za Ligi Kuu ya msimu ujao wa 2018-2019.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA SAMATTA YAREJEA LIGI KUU, FRIENDS RANGERS HAIKUWA BAHATI YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top