• HABARI MPYA

  Sunday, February 04, 2018

  SUDAN WAMALIZA NAFASI YA TATU CHAN 2018 MOROCCO

  TIMU ya taifa Sudan imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa penalty 4-2 kufuatia sare ya 1-1 na Libya jana Uwanja wa Marrakech.
  Baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, Sudan wakitangulia kwa bao la Waala Musa dakika ya nane kabla ya Salem Ablo kuisawazishia Libya dakika ya 84, kipa Akram El Hadi Salim akaenda kuwa shujaa kwenye mikwaju ya penalti.
  Waliofunga penalti za Sudan inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba SC ya Tanzania, Mcroatia ni Zdravko Lograrocic ni Tajeldin Elnour, Samawal Nour, Ahmad Adam Mohammad na Maaz Gismalla wakati za Libya zilifungwa na Meftah Taqtaq na Abdulsalam Omar.
  Akram akaibuka shujaa wa Sudan baada ya kuokoa mikwaju ya penalti ya Elmehdi Elhouni na Salem Ablo.
  CHAN 2018 inahitimishwa leo kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji Morocco na Nigeria Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca kuanzia Saa 4:00 usiku, mchezo ambao kwa hapa Tanzania utaonyeshwa na chaneli ya ZBC 2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SUDAN WAMALIZA NAFASI YA TATU CHAN 2018 MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top