• HABARI MPYA

  Wednesday, February 07, 2018

  SIMBA SC YAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUZIDI KUUKARIBIA UBINGWA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi.
  Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. 
  Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okiw (kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee leo
  Mganda Emmanuel Okwi akiwatoka walinzi wa Azam FC, Mghana Yakubu Mohammed (kulia) na Mcameroon Stephane Kingue (katikati)
  Kiungo wa Simba, Said Ndemla akimtoka winga Mghana wa Azam, Enock Atta0Agyei
  Beki Mghana wa Azam FC, Daniel Amoah akimiliki mpira dhidi ya mshambuliaji wa Simba, John Bocco
  Wachezaji wa timu zote mbili wakitoka kuingia uwanjani leo

  Dalili za Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma kupata bao zilionekana mapema tu mchezo huo ulipoanza kutokana na mashambulizi yake mfululizo langoni mwa wapinzani.
  Azam FC walizidiwa katika safu ya kiungo na kujikuta wanawapa fursa Simba kutawala mchezo sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza.
  Benchi la Ufundi la Azam chini ya Mromania, Aristica Cioaba ba mzalendo, Iddi Cheche liliona hilo na mapema kipindi cha pili wakamuingiza kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Iddi Kipagwile.
  Mabadiliko hayo yaliipa uhai Azam FC na kuanza kupeleka mashambulizi makali langoni mwa Simba, lakini kipa namba moja nchini, Aishi Manula alisimama imara kuokoa akisaidiwa na mabeki, Yussuph Mlipili na Erasto Nyoni.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Yussuph Mlipili, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk59, John Bocco, Emmanuel Okwi/Nicholaus Gyan dk84 na James Kotei.
  Azam FC; Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Iddi Kipagwile/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk55, Frank Domayo, Mbaraka Yussuph, Yahya Zayed/Bernard Arthur dk71 na Enock Atta-Agyei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUZIDI KUUKARIBIA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top