• HABARI MPYA

  Friday, February 09, 2018

  SERIKALI YAMTEUA TENGA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BMT, KIGANJA KATIBU TENA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrisons Mwakyembe amemteua Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT).
  Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lorietha Laurence imesema kwamba amewateua Wajumbe tisa, wakiwemo watumishi watatu wa Wizara yake kuingia kwenye Baraza hilo.
  Leodegar Chilla Tenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa BMT

  Kutokana Wizarani wateule ni Yussuph Singo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Dk. Edicome Shirimam, Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi na Mohammed Kiganja, ambaye atakuwa Katibu wa Baraza hilo kwa mara nyingine tena.
  Wajumbe wateule wengine sita ni kutoka sehemu mbalimbali ambao ni Profesa Mkumbwa Mtambo, Betrice Singano, Kanali Mstaafu, Juma Ikangaa, Mbunge na Mwanasheria Damas Ndumbaro, Rehema Seif Madenge na Salmin Kaniki.
  Uteuzi huu unakuja baada ya Waziri Mwakyembe kuuvunja uongozi uliopita wa BMT uliokuwa chini ya Dioniz Malinzi Julai mwaka jana na kuipa Sekretarieti chini ya Kiganja jukumu la kuongoza hadi utakapoteuliwa uongozi mpya.
  Pamoja na hayo, Waziri Mwakyembe amemteua Timoth Mganga kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAMTEUA TENGA KUWA MWENYEKITI MPYA WA BMT, KIGANJA KATIBU TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top