• HABARI MPYA

    Sunday, February 04, 2018

    SAMATTA ACHEZA VIPINDI VYOTE GENK YASHINDA 1-0 UGENINI UBELGIJI

    Na Mwandishi Wetu, MOUSCRON
    NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza kwa dakika 68, timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 1-0 ugenini katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji dhidi ya wenyeji, Royal Excel Mouscron Uwanja Le Canonnier mjini Mouscron, Ubelgiji.
    Samatta alimpisha mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Dieumerci N'Dongala aliyekwenda kufunga bao pekee la ushindi katika mchezo huo dakika ya 83.  
    Samatta leo alikuwa anacheza kwa mara ya pili tangu apone maumivu ya mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia iliyochanika Novemba 4, mwaka jana akiichezea KRC Genk ikilazimishwa sare ya 0-0 na Lokeren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk na kumsababisha afanyiwe upasuaji mdogo. 
    Mbwana Samatta akipambana jana Uwanja Le Canonnier mjini Mouscron katika mechi dhidi ya Royal Excel Mouscron  

    Mechi ya kwanza ilikuwa ya Ligi pia, ambayo aliingia dakika saba za mwisho kuchukua nafasi ya Mkosovo Edon Zhegrova, Genk ikilazimishwa sare ya 1-1 na Sint-Truiden Januari 27 Uwanja wa Luminus Arena kabla ya jana kuanza hadi dakika ya 75 alipompisha Zhegrova.
    Akarudi uwanjani Jumanne wiki hii na kutoa pasi ya bao la kwanza la timu yake, KRC Genk ikifungwa 3-2 na wenyeji, Kortrijk katika mechi ya Kombe la Ubelgiji Guldensporen mjini Kortrijk.
    Samatta alimsetia mshambuliaji Marcus Ingvartsen kuifungia bao la kwanza Genk dakika ya 17, kabla ya kiungo Mnigeria, Abdul Ajagun kuwasawazishia wenyeji dakika ya 23 na kiungo mwingine, Mfaransa Larry Azouni akafunga la pili dakika ya 36.
    Wakati kipindi cha kwanza kikikaribia kabisa kumalizika, Genk wakasawazisha kupitia kwa kiungo Mbelgiji, Thomas Buffel dakika ya 45 na ushei.
    Kipindi cha pili, wenyeji, Kortrijk wakamaliza kazi kwa lao tatu la beki Mfaransa, Lucas Rougeaux dakika ya 88 na sasa timu hizo zitarudiana Februari 6 nyumbani kwa Genk, Luminus Arena.
    Samatta amefikisha mechi 73 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
    Remedial : Werner, Huyghebaert, Mézague, Galitsios/Van Durmen dk19, Godeau, De Medina, Govea, Mohamed, Rotariu/Awoniyi dk57, Olinga/Debaisieux dk86 na Bolingi.
    KRC Genk: Vukovic, Uroon, Colley, Dewaest, Nastic, Wouters, Seck, Pozuelo/Aidoo dk86, Samatta/Ndongala dk68, Buffel na Ingvartsen/Karelis dk71.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA VIPINDI VYOTE GENK YASHINDA 1-0 UGENINI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top