• HABARI MPYA

  Saturday, February 03, 2018

  NINJA WA JANGWANI NJE MWEZI MZIMA KWA MAUMIVU YA KISIGINO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kati wa Yanga SC, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (pichani kushoto) atakuwa nje kwa mwezi mmoja kutokana na maumivu ya kisigono cha mguu wa kushoto.
  Daktari wa Yanga, Edward Bavu amesema kwamba baada ya uchunguzi wa kitabibu aliofanyiwa mchezaji huyo chipukizi imegundulika maumivu yake tanahitaji mapumziko ua takriban mwezi mmoja.
  Bavu amesema kwamba mchezaji huyo aliumia wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na baada ya kuona anachukua muda mrefu kupona kufuatia tiba za awali, wakaamua kumfanyia vipimo.   
  "Atakuwa nje kwa wiki tatu au nne, aliumua wakati wa mashindano ya kombe la Mapinduzi, awali tulijua ni tatizo dogo lakini baada ya uchunguzi wa kina tumegundua kuwa Kunatatizo kwenye kisingino na kifundo cha mguu wa kushoto,”amesema Dk. Bavu.
  Ninja yupo katika msimu wake wa kwanza Yanga SC baada ya kusajiliwa Juni mwaka jana kutoka Taifa Jang'ombe ya Zanzibar.
  Kwa aina ya uchezaji wake na umbo lake, Yanga inaamini kabisa Ninja atakuwa mrithi wa muda mrefu wa Nahodha wao, beki wa kati aliyedumu Jangwani tangu mwaka 2006, Nadir Haroub ‘Cannavaro’. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NINJA WA JANGWANI NJE MWEZI MZIMA KWA MAUMIVU YA KISIGINO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top