• HABARI MPYA

  Monday, February 05, 2018

  NI MOROCCO MABINGWA WA CHAN 2018, NIGERIA YAFA 4-0 CASABLANCA

  WENYEJI Morocco wamefanikiwa kutwaa Kombe la Fainali za Ubingwa wa Michuano ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nigeria 4-0 Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca.
  Ushindi huo umetokana na mabao ya Zakaria Hadraf mawili, Walid El Karti na Ayoub El Kaabi moja kila mmoja na Morocco wanabeba tena Kombe kubwa la Afrika kwa mara ya kwanza tangu walipochukua Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1976.
  Wenyeji jana walikuwa bora mno zaidi ya Nigeria waliozidiwa kabisa baada ya Peter Eneji Moses kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 48.
  Winga wa kushoto, Ismail Haddad alikuwa nyota mchezo wa jana kwenye michuano inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya kusaidia upatikanaji wa mabao matatu.
  Zakaria Hadraf alifunga bao la kwanza dakika ya 45 na la tatu dakika ya 64, Walid El Karti akafunga la pili dakika ya 61 na Ayoub El Kaabi la nne dakika ya 73.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MOROCCO MABINGWA WA CHAN 2018, NIGERIA YAFA 4-0 CASABLANCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top