• HABARI MPYA

  Monday, February 05, 2018

  MEXIME AKALIA KUTI KAVU KAGERA SUGAR...TIMU IMESHINDA MECHI MBILI TU MSIMU MZIMA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  KIPIGO cha mabao 2-1 cha Kagera Sugar kutoka kwa wenyeji Mbao FC jana Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kinazidi kumuweka pagumu kocha Mecky Mexime.
  Mabao ya Mbao FC yalifungwa na James msuva dakika ya 63 na Habib Kiyombo dakika ya 70, wakati la Kagera Sugar lilifungwa na Atupele Green dakika ya 74.
  Matokeo hayo yanazidi kuididimiza Kagera Sugar sasa ikiangukia nafasi ya 16 katika Ligi Kuu ya 16, kutokana na pointi zake 13 za mechi 16, wakati Mbao FC inajisogeza nafasi ya saba baada ya kufikisha pointi 18.
  Kagera Sugar imeshinda mechi mbili tu za Ligi Kuu msimu huu kati ya 16 ilizocheza, nyingine ikifungwa saba na kutoa sare saba. Na imetolewa hatua ya 32 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kufungwa 2-0 na Buseresere FC nyumbani Uwanja wa Kaitaba Bukoba.
  Mechi ilizoshinda Kagera Sugar msimu huu ni dhidi ya Ndanda FC 2-1 Oktoba 29 Uwanja wa Kaitaba na dhidi ya Mtibwa Sugar Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Manungu Turiani, Morogoro.
  Ilizofungwa ni dhidi ya Mbao FC mara mbili, mbali na jana walipigwa pia 1-0 Agosti 26, 2017 Kaitaba, wapigwa 1-0 na Azam FC Septemba 15 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, wakapigwa 1-0 na Singida United Septemba 24 Uwanja wa Namfua, Singida kabla ya kupigwa na Yanga 2-1 Uwanja wa Kaitaba.
  Kagera walifungwa pia 1-0 na Njombe Mji FC Januari 15 Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe , wakapigwa 2-0 na Simba SC Uwanja wa Kaitaba kabla ya jana kuchapwa 2-1 na Mbao jana Kirumba.
  Wametoa sare na Ruvu Shooting 1-1 Kaitaba Septemba 10, wametoa sare ya 0-0 na Maji Maji mjini Songea Septemba 30, wametoa sare ya 1-1 na Mwadui FC mjini Shinyanga Oktoba 20, wametoa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Kaitaba Novemba 14, wametoa sare ya 0-0 na Stand United Novemba 25, wametoa sare ya 0-0 na Mbeya City Januari 2 na sare ya 0-0 tena na Lipuli Kaitaba, Bukoba.
  Kwa matokeo haya, wazi Kagera Sugar inachungulia njia ya kuelekea Daraja la Kwanza kama haitasimama imara na kuanza kukusanya pointi mfululizo katika mechi zake zijazo.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu jana, mabao ya Nahodha John Raphael Bocco mawili moja kila la kipindi na kiungo Muzamil Yassin kipindi cha pili, yaliipa Simba SC ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa UHuru, Dar es Salaam.
  Nayo Mtibwa Sugar ikachezea kichapo cha 2-1 kutoka kwa wenyeji Stand United Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Mabao ya Stand United yalifungwa na Birigamana Babikakule dakika ya 79 na Tariq Seif dakika ya 87 wakati la Mtibwa Sugar lilifungwa na Salum Kihimbwi dakika ya 25.
  Kipigo cha Mbao FC jana kinazidi kumuweka mahali pabaya kocha Mecky Mexime wa Kagera Sugar

  MATOKEO YA KAGERA SUGAR MSIMU HUU 
  Agosti 26, 2017; Kagera Sugar 0-1 Mbao FC
  Septemba 10, 2017; Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
  Septemba 15, 2017; Azam FC 1-0 Kagera Sugar
  Septemba 24; 2017; Singida United 1-0 Kagera Sugar
  Septemba 30, 2017; Maji Maji  0-0 Kagera Sugar
  Septemba 14, 2017; Kagera Sugar 1-2 Yanga SC
  Oktoba 20, 2017; Mwadui FC 1-1 Kagera Sugar
  Oktoba 29, 2017; Kagera Sugar 2-1 Ndanda FC
  Novemba 4, 2017; Kagera Sugar 1-1 Tanzania Prisons
  Novemba 19, 2017; Mtibwa Sugar 0-1 Kagera Sugar
  Novemba 25, 2017; Kagera Sugar 0-0 Stand United
  Januari 2, 2018; Mbeya City 0-0 Kagera Sugar
  Januari 15, 2018; Njombe Mji 1-0 Kagera Sugar
  Januari 22, 2018; Kagera Sugar 0-2 Simba
  Januafri 27, 2018; Kagera Sugar 0-0 Lipuli
  Februari 4, 2018; Mbao FC 2-1 Kagera Sugar
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MEXIME AKALIA KUTI KAVU KAGERA SUGAR...TIMU IMESHINDA MECHI MBILI TU MSIMU MZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top