• HABARI MPYA

  Friday, February 09, 2018

  MECHI ZA RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA ZAANZA LEO

  RAUNDI ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika inaanza leo kwa mechi mbili tu, zote zikichezwa nchini Mali.
  Djoliba FC wataikaribisha ELWA United ya Liberia Uwanja wa Machi 26 mjini Bamako, wakati Onze Createurs watakuwa wenyeji wa CR Belouizdad ya Algeria.
  Mechi zaidi za hatua hii zinatarajiwa kuchezwa kesho, Petro Atletico ya Angola ikiikaribisha Masters Security ya Malawi, Young Buffaloes ya Swaziland ikiikaribisha Cape Town City ya Afrika Kusini, Costa do Sol ya Msumbiji na Jwaneng ya Botswana, Energie ya Benin Hafia ya Guinea na Ngazi Sport ya Comoro watawaalika Port Louis ya Mauritius.
  Mangasport ya Gabon watakuwa wenyeji wa Maniema Union ya DRC, Olympic Star ya Burundi na Etoile Filante ya Burkina Faso, New Stars ya Cameroon na Deportivo Niefang ya Equatorial Guinea, Tanda ya Ivory Coast na CS la Mancha ya Kongo, Al Ittihad ya Libya na Sahel ya Niger, US Ben Guerdane ya Tunisia na Hilal Juba ya Sudan Kusini, El Masry ya Misri na Green Buffaloes ya Zambia.
  Mechi za kwanza za raundi hii zitakamilishwa Jumapili kwa APR kuwakaribisha Anse Reunion ya Shelisheli, Akwa United ya Nigeria na Hawks ya Gambia, Asante Kotoko ya Ghana na CARA ya Kongo, AFC Leopards ya Kenya na FOSA Juniors ya Madagascar, Simba ya Tanzania na Gendarmerie ya Djibouti, RS Berkane ya Morocco na Mbour Petite Cote ya Senegal, Africa Sports ya Ivory Coast na FC Nouadhibou ya Mauritania na Zimamoto ya Zanzibar dhidi ya Wolaitta Dicha (Ethiopia).
  Ikumbukwe mshindi kati ya El Masry inayofundishwa gwiji wa Misri, Hossam Hassan na Green Buffaloes atakutana na mshindi kati ya Simba SC na Gendarmerie.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI ZA RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA ZAANZA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top