• HABARI MPYA

  Wednesday, February 07, 2018

  LUIS ENRIQUE AKARIBIA KUCHUKUA NAFASI YA CONTE CHELSEA

  KOCHA Luis Enrique anaonekana yuko tayari kuchukua nafasi ya Antonio Conte klabu ya Chelsea huku taarifa nchini Hispania zikisema kwamba kocha huyo wa zamani wa Barcelona tayari amekubaliana na timu hiyo ya London.
  Nafasi ya Conte kubaki The Blues ni finyu baada ya vipigo mfululizo vya 3-0 nyumbani mbele ya Bournemouth na baada kupigwa 4-1 na Watford Jumatatu.
  Na kutokana na Chelsea kujiweka kwenye mazingira magumu ya kumaliza kwenye nafas nne za juu, mmiliki Roman Abramovich anaweza kulazimisha hatua ichukuliwe mara moja.
  Kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique amekubali kujiunga na Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Na taarifa zinasema anaweza kumpa kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 mkataba wa ambao utamalizika mwaka 2020.
  Enrique, ambaye pia amewahi kufundisha Roma na Celta Vigo, yuko huru baada ya kuondoka Barcelona msimu uliopita, wakati alipokuwa Nou Camp aliiongoza Barca kutwaa mataji mawili ya La Liga, matatu ya Copa del Rey triumphs and glory in the 2015 Champions League final. 
  Mechi ya kwanza yla Enrique baada Februari 20, kabla ya kusafiri hadi Katalunia Machi 14 kwa mchezo wa marudiani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUIS ENRIQUE AKARIBIA KUCHUKUA NAFASI YA CONTE CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top