• HABARI MPYA

  Friday, February 09, 2018

  KOCHA SIMBA SC: SIJAONA NAMBA SITA BORA KAMA MKUDE TANZANIA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KOCHA Msaidizi wa Simba SC, Mrundi Masoud Juma amesema kwamba hajaona namba sita bora zaidi ya kiungo wa klabu yake, Jonas Gerald Mkude.
  Juma aliyasema hayo juzi baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salam – Simba SC ikiibuka na ushindi wa 1-0, bao pekee la mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi.  
  “Kwangu mimi, Tanzania hakuna namba sita mzuri kama Jonas Mkude, nasema kwangu mimi, nchi hii hakuna namba sita mzuri kama Mkude. Anajituma, anafanya kila kitu uwanjani kuisaidia timu kushinda,”alisema.
  Jonas Mkude (kulia) ameitendea haki heshima aliyopewa na makocha wake Simba SC 

  Jonas Mkude amekuwa na wakati mzuri tena Simba SC baada ya ujio wa Mrundi huyo Novemba mwaka jana, kufuatia kuanza kupoteza nafasi yake kikosi cha kwanza chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog aliyeondolewa Desemba mwaka jana.
  Juma amemuaminisha hata kocha mpya Mkuu wa Simba SC, Mfaransa Pierre Lechantre juu ya Mkude, zao la kikosi cha vijana cha Wekundu wa Msimbazi, ambaye naye ameendelea kumtumia katika nafasi ya kiungo wa ulinzi.
  Na Mkude ameitendea haki heshima hiyo kwa kucheza vizuri hata kuisaidia Simba kuwa na ukuta mgumu bila kujali amepangwa na mabeki, au kipa gani.   
  Masoud Juma (kushoto) anaamini Tanzania hakuna namba sita bora zaidi ya Jonas Mkude 
  Kocha mpya Mkuu wa Simba SC, Mfaransa Pierre Lechantre (kushoto) naye ameamini Jonas Mkude ni bora
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA SIMBA SC: SIJAONA NAMBA SITA BORA KAMA MKUDE TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top