• HABARI MPYA

    Friday, February 09, 2018

    KAGERA SUGAR SASA KATIKA ANGA ZA KUSHUKA DARAJA BAADA YA KICHAPO CHA RUVU

    Na Mwandishi Wetu, MWANZA
    KIPIGO cha mabao 2-0 cha Kagera Sugar kutoka kwa wenyeji Ruvu Shooting Alhamisi Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kimeifikisha timu hiyo kwenye eneo rasmi kuteremka daraja.
    Mabao ya Ruvu Shooting yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 55 na Alinanuswe Martin dakika ya 79.
    Matokeo hayo yanaifanya Kagera Sugar ibaki na pointi zake 13 baada ya mechi 17, hivyo kuhamia nafasi ya 15 katika Ligi Kuu ya timu 16 ambayo mwishoni mwa msimu itateremsha timu mbili.
    Kagera Sugar inalingana kwa pointi na Njombe Mji FC inayoshika mkia kutokana na kuzidiwa tu wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Ruvu Shooting yenyewe inapanda hadi nafasi ya 12, ikifikisha pointi 17 sawa na Ndanda FC iliyo juu yao kwa wastani wa mabao baada ya timu zote kucheza mechi 17.  
    Kagera Sugar wameshinda mechi mbili tu za Ligi Kuu msimu huu kati ya 17 walizocheza hadi sasa

    Kagera Sugar imeshinda mechi mbili tu za Ligi Kuu msimu huu kati ya 17 ilizocheza, nyingine ikifungwa nane na kutoa sare saba. Na imetolewa hatua ya 32 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kufungwa 2-0 na Buseresere FC nyumbani Uwanja wa Kaitaba Bukoba.
    Mechi ilizoshinda Kagera Sugar msimu huu ni dhidi ya Ndanda FC 2-1 Oktoba 29 Uwanja wa Kaitaba na dhidi ya Mtibwa Sugar Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Manungu Turiani, Morogoro.
    Ilizofungwa ni dhidi ya Ruvu Shooting 2-0 Alhamisi, Mbao FC mara mbili, mbali na jana walipigwa pia 1-0 Agosti 26, 2017 Kaitaba, wapigwa 1-0 na Azam FC Septemba 15 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, wakapigwa 1-0 na Singida United Septemba 24 Uwanja wa Namfua, Singida kabla ya kupigwa na Yanga 2-1 Uwanja wa Kaitaba.
    Kagera walio chini ya kocha Mecky Mexime Sililia Kianga, ilifungwa pia 1-0 na Njombe Mji FC Januari 15 Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe , wakapigwa 2-0 na Simba SC Uwanja wa Kaitaba kabla ya jana kuchapwa 2-1 na Mbao jana Kirumba.
    Wametoa sare na Ruvu Shooting 1-1 Kaitaba Septemba 10, wametoa sare ya 0-0 na Maji Maji mjini Songea Septemba 30, wametoa sare ya 1-1 na Mwadui FC mjini Shinyanga Oktoba 20, wametoa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Kaitaba Novemba 14, wametoa sare ya 0-0 na Stand United Novemba 25, wametoa sare ya 0-0 na Mbeya City Januari 2 na sare ya 0-0 tena na Lipuli Kaitaba, Bukoba.
    Kwa matokeo haya, wazi Kagera Sugar inachungulia njia ya kuelekea Daraja la Kwanza kama haitasimama imara na kuanza kukusanya pointi mfululizo katika mechi zake zijazo.
    Ruvu Shooting wamejiondoa mkiani baada ya ushindi wa Alhamisi dhidi ya Kagera Sugar

    MATOKEO YA KAGERA SUGAR MSIMU HUU 
    Agosti 26, 2017; Kagera Sugar 0-1 Mbao FC
    Septemba 10, 2017; Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
    Septemba 15, 2017; Azam FC 1-0 Kagera Sugar 
    Septemba 24; 2017; Singida United 1-0 Kagera Sugar
    Septemba 30, 2017; Maji Maji  0-0 Kagera Sugar
    Septemba 14, 2017; Kagera Sugar 1-2 Yanga SC
    Oktoba 20, 2017; Mwadui FC 1-1 Kagera Sugar
    Oktoba 29, 2017; Kagera Sugar 2-1 Ndanda FC  
    Novemba 4, 2017; Kagera Sugar 1-1 Tanzania Prisons
    Novemba 19, 2017; Mtibwa Sugar 0-1 Kagera Sugar
    Novemba 25, 2017; Kagera Sugar 0-0 Stand United
    Januari 2, 2018; Mbeya City 0-0 Kagera Sugar
    Januari 15, 2018; Njombe Mji 1-0 Kagera Sugar 
    Januari 22, 2018; Kagera Sugar 0-2 Simba
    Januafri 27, 2018; Kagera Sugar 0-0 Lipuli
    Februari 4, 2018; Mbao FC 2-1 Kagera Sugar
    Februari 8, 2018; Ruvu Shooting 2-0 Kagera Sugar
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR SASA KATIKA ANGA ZA KUSHUKA DARAJA BAADA YA KICHAPO CHA RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top